Abdi Ahmed Mohamud ateuliwa Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC

Tom Mathinji
1 Min Read
Abdi Ahmed Mohamud ateuliwa Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC.

Tume ya Maadili na kukabiliana na Ufisadi EACC, imemteua Abdi Ahmed Mohamud kuwa Afisa Mkuu Mtendaji.

Hadi kuteuliwa kwake, Ahmed alikuwa naibu Afisa Mkuu Mtendaji, na iwapo uteuzi wake utaidhinishwa na bunge, atachukua nafasi iliyoshikiliwa na Twalib Mbarak anayeondoka.

Uteuzi wa Ahmed ulitangazwa Ijumaa kupitia arifa iliyoandikwa na mwenyekiti wa tume hiyo David Oginde.

Kabla ya kuchukua wadhifa wa naibu afisa mkuu mtendaji wa EACC, Ahmed alihudumu kama mkurugenzi wa kitengo cha uchunguzi katika tume hiyo.

Tume hiyo ilikuwa imetangaza nafasi hiyo kuwa wazi na kuwataka wanaopania kuchukua nafasi hiyo kuwasilisha maombi kupitia tovuti yake na magazeti ya humu nchini mnamo tarehe 17 mwezi Septmba mwaka huu.

Watu 172, walituma maombi kujaza nafasi hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *