Wanyama wote; Chui,Papa na Sofapaka wafumwa ligini

Dismas Otuke
1 Min Read

AFC Leopards maarufu kama chui,Kariobangi Sharks na Sofapaka AKA Batoto Ba Mungu, wamepoteza mechi za ligi kuu Kenya FKF za raundi ya kumi   zilizochezwa Jumamosi katika nyuga mbalimbali.

Katika uwanja wa Kasarani Chui wameambulia kichapo cha mabao 3-2  dhidi ya Nairobi City Stars,Vincent Owino,Samuel Kapen na Robinson Asenwa wakipachika moja kila moja kwa City huku Brian Yakhama na Victor Otieno wakifunga  magoli ya kufutia machozi kwa Ingwe.

Wachezaji wa City Stars wakisherehekea bao dhidi ya AFC Leopards 

Ugani Sudi Nzoia Sugar wamerejelea tambo za ushindi baada ya kuwanyofoa Kariobangi Sharks goli moja kwa sifuri,Emmanuel Osoro akiwafungia wenyeji bao pekee na la ushindi katika dakika ya 90.

Talanta FC wakimenyana na Kariobangi Sharks uwanjani Sudi

Katika uwanja wa kaunti ya Machakos wageni  Talanta FC wamekosa adabu za mgeni walipoidhalilisha Sofapaka kwa kichapo cha tatu bila.

Share This Article