Wataalamu wa lishe bora wakongamana Nairobi

Marion Bosire
1 Min Read
Dr. David Okeyo, KNDI

Wataalamu wa lishe bora pamoja na watafiti wanakutana jijini Nairobi kuanzia leo kwa kongamano la siku nne la kuchunguza mifumo ya chakula na usawa wa lishe hapa nchini.

Kongamano hilo kupitia taasisi ya wataalamu wa lishe bora na chakula hapa nchini-KNDI linawaleta pamoja wataalam wa masuala ya chakula kutoka kanda hii kujadili suala la ukosefu wa usawa katika mifumo ya chakula, hali ambayo huchangia lishe duni.

Mkurugenzi wa taasisi ya KNDI, Dkt David Okeyo amesema ipo haja kwa wakenya kupunguza ulaji wa nafaka na badala yake kula vyakula vyenye afya kama vile matunda na mboga.

Dkt Okeyo alitoa wito kwa watekelezaji sera kushughulikia dosari zilizopo katika mifumo ya chakula hasusan maskini katika jamii.

Kauli mbiu ya mkutano huo wa tatu wa kimataifa ni ‘mifumo endelevu ya chakula, lishe, ukosefu wa usawa wa kiafya na sera’.

Website |  + posts
Share This Article