Mapato katika sekta ya mboga na matunda yaongezeka

Tom Mathinji
1 Min Read

Kenya ilipata zaidi ya shilingi bilioni 140 kutokana na  mauzo ya bidhaa za mboga, matunda na maua mwaka 2022, huku maua pekee ikileta mapato ya shilingi bilioni 100.

Waziri wa kilimo, ustawi wa mifugo na uvuvi Mithika Linturi, alisema ufanisi huo ulitokana na sera mwafaka zilizowekwa na serikali, pamoja na utoaji wa mbolea ya bei nafuu, hatua iliyovutia wadau wengi katika sekta hiyo.

Kulingana na Waziri hiyo, mapato hayo ni ongezeko ikilinganishwa na mapato yaliyonakiliwa katika kipindi sawa na hicho mwaka uliopita.

Waziri alisema serikali itaendelea kutoa vishawishi kwa wakulima ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za nyanjani za kilimo ili kuongeza uzalishaji.

Alidokeza kuwa serikali ina mipango ya kupanua uwanja wa ndege wa Eldoret ili utumike kusafirisha bidhaa za kilimo nje ya nchi, huku bandari ya Mombasa ikitumika kusafirisha maua.

Akizungumza wakati wa ufungu,I wa maonyesho ya bidhaa za mboga, matunda na maua Naivasha, Waziri huyo alisema serikali imejitolea kupiga jeki sekta hiyo kwani ni mojawepo wa sekta zilizo na mapato ya juu nchini katika sekta ya uuzaji bidhaa nje ya nchi.

Sekta ya bidhaa za mboga, matunda na maua hapa nchini, imewaajiri takribani watu milioni 6.5 moja Kwa moja au kupitia njia zingine.

Website |  + posts
Share This Article