Mahakama ya Hakimu Mkuu ya Mombasa, inatarajiwa kutoa uamuzi leo Ijumaa kuhusu kesi ya mauaji ya watoto inayomkabili mhubiri anayekumbwa na utata Paul Mackenzie, pamoja na washtakiwa wenza 94, akiwemo mke wake Rhoda Mumbua Maweu.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 238 za mauaji bila kukusudia, ambapo wanadaiwa waliwalazimisha waathira kutokula chakula ama kunywa vinwaji hadi kufa, katika msitu wa shakahola kati ya mwezi Januari mwaka 2021 na mwezi Septemba mwaka 2023.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkuu Alex Ithuku.
Siku ya Alhamisi Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Mahakama ya Shanzu, Leah Juma, alimpata Mackenzie na hatia katika mashtaka yote matano ya ugaidi na itikadi kali, ikiwemo shughuli za uhalifu uliopangwa, itikadi kali, kuwezesha kitendo cha kigaidi, na kumiliki machapisho ya kigaidi, huku maelekezo ya adhabu yakipangwa tarehe 25 Januari 2027.