Wanajeshi 13 wa Niger wauawa kwenye shambulizi la kigaidi

Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya taifa hilo, shambulizi hilo lilitekelezwa siku ya Alhamisi na watu wasiojulikana.

Tom Mathinji
1 Min Read
Wanajeshi 13 wa Niger wauawa kwenye shambulizi la kigaidi.

Takriban wanajeshi wasiopungua 13 wa  Niger waliuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi kwenye kambi yao eneo la  Sanam, Tillabéri magharibi mwa Niger.

Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya taifa hilo, shambulizi hilo lilitekelezwa siku ya Alhamisi na watu wasiojulikana.

Shambulizi hilo lilitokea alfajiri huko Sanam, karibu na mpaka wa Mali, eneo ambalo limekuwa likikumbwa na mashambulizi ya makundi yenye silaha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, vikosi vya usalama  vilisema viliwaua washambuliaji kadhaa, vikatibua miundombinu yao, na vinaendelea na operesheni ya kuwasaka waliohusika huku majeruhi wakipelekwa hospitalini.

Tukio hili limetokea siku mbili baada ya wanajeshi 11 wa Niger kuuawa katika shambulio linalohusishwa na kundi la Boko Haram huko Baroua, eneo la Diffa kusini-mashariki mwa nchi hiyo

Sio bayana ni nani alitekeleza shambulizi hilo.

TAGGED:
Share This Article