Wanajeshi wawili wa Libya walifariki kwenye shambulizi lililotekelezwa na Ukraine dhidi ya meli ya Urusi katika bandari ya Benghazi.
Serikali ya Libya imesema kuwa, watu 10 pia walijeruhiwa katika shambulizi hilo la Jumapili ambalo lilitekelezwa na ndege isiyo na rubani.
Shambulizi hilo limekashifiwa vikali na maafisa wa Libya na Shirika la Umoja wa Mataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha, alitetea shambulizi hilo, akidokeza kuwa Ukraine inaheshimu uhuru wa Libya, na haikuwa na nia yoyoe ya kusababisha madhara kwa Libya.
“Ukraine haina lengo la kuhamisha vita kwingineko,” alisema Sybiha kupitia mtandao wa Telegram.
Kulingana na waziri huyo, Russia ndiyo inahatarisha mataifa yanayostawi kwa kuwatumia wananchi wa nchi hizo kwa shughuli za kivita.