Mwigizaji mkongwe wa Nollywood Pete Edochie amefariki

Kulingana na taarifa ya familia yake kwenye mtandao wa Instagram,  Edochie alifariki  Jumatano alfajiri.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwigizaji mkongwe wa Nollywood Pete Edochie amefariki.

Mwigizaji mkongwe wa Nollywood Pete Edochie, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 79 baada ya kuugua kwa muda mrefu saratani ya uzazi.

Kulingana na taarifa ya familia yake kwenye mtandao wa Instagram,  Edochie alifariki  Jumatano alfajiri.

“Tunapoomboleza kifo cha mpendwa wetu, tunamuomba Mungu ampumzishe mahali pema, na atupatie nguvu wakati huu wa msiba,” ilisema taarifa ya familia.

Edochie amemwacha mke wake Josephine Edochie, watoto, pamoja na ndugu zake.

Famiia yake ilisema mipango ya mazishi itatangazwa baadaye.

Pete Edochie alizaliwa tarehe 7 mwezi Machi 1947, eneo la Zaria, jimbo la Kaduna State.

Alisomea taaluma ya uanahabari na televisheni nchini Uingereza.

Alijiunga na Shirika la Utangazaji la Eastern Nigeria mwaka 1967, ambako alipanda madaraka kutoka mwelekezi wa vipindi hadi Naibu Mkurugenzi Mkuu.

Share This Article