Serikali yaongeza shilingi bilioni 5 kwa hazina ya hustler

Rais Ruto alidokeza kuwa hatua hiyo itawezesha hazina hiyo kuimarisha uchumi miongoni mwa wananake na vijana nchini Kenya.

Tom Mathinji
1 Min Read
William Ruto - Rais wa Kenya.

Serikali imetangaza kupiga jeki hazina ya hustler kwa kuongeza shilingi bilioni tano zaidi, ili kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali za kutosha za mkopo.

Akitangaza hayo, Rais William Ruto, alidokeza kuwa hatua hiyo pia itawezesha hazina hiyo kuimarisha uchumi miongoni mwa wananake na vijana nchini Kenya.

Wakati huo huo, kiongozi wa taifa aliagiza kuongezwa kwa kiwango cha mkopo kwa takriban watu milioni 4.5 ambao hutumia hazina, ambayo huto mkopo kwa mtu binafsi ya hadi shilingi 150,000.

Aidha, Rais Ruto aliwahimiza wasimamizi wa hazina hiyo kubuni mfumo ambapo makundi yanaweza pata fedha na kutoa mkopo kwa wanachama wao.

Rais Ruto aliyasema hayo Jumanne wakati wa maadhimisho  ya 17 tangu kuanzishwa kwa shirika la Joyous Women, JOYWO katika Ikulu ya Nairobi.

Kwenye hafla hiyo, Ruto alitoa wito kwa wanawake kutumia vyema shilingi bilioni 2 walizotengewa na serikali kwenye kandarasi za manunuzi.

Share This Article