Senegal imerejeshewa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya bara Afrika (AFCON) mwaka 2025 kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).
Uamuzi huo wa mahakama wa kuirejesha Senegal kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025, umebatilisha uamuzi wa awali wa Shirikisho la Soka Afrika bara Afrika (CAF), ulioipokonya Senegal taji hilo na kulikabidhi wenyeji Morocco katika fainali ya kusisimua iliyochezwa jijini Rabat mwezi Januari.
Senegal ilikuwa imetangazwa bingwa baada ya kuifunga Morocco bao 1-0 katika muda wa nyongeza wa fainali iliyochezwa Rabat.
Hata hivyo, CAF ilibatilisha matokeo hayo mwezi Machi na kuipa Morocco ushindi wa mabao 3-0 kwa madai kwamba Senegal ilikiuka kanuni za mashindano kwa kuondoka uwanjani wakati wa dakika za nyongeza za kipindi cha pili, kupinga penalti iliyokuwa imetolewa kwa wenyeji Morocco.
Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) liliwasilisha rufaa kwa CAS kupinga uamuzi huo, likisisitiza kuwa adhabu iliyotolewa na CAF haikuwa sahihi.
Uamuzi huo sasa unairejeshea Teranga Lions hadhi ya mabingwa wa Afrika wa mwaka 2025, na hivyo kumaliza mzozo uliozua utata mkubwa na kufunika mafanikio ya mashindano hayo.