Tamasha ya kitaifa ya kusherehekea miaka 30 ya muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania inatarajiwa kufanyika mjini Kahama, katika Mkoa wa Shinyanga, Ijumaa, Novemba 27, 2026.
Hafla hiyo itafanyika katika ukumbi wa Malex na kuwakutanisha wasanii waliowahi kuasisi muziki huo pamoja na wanamuziki wa kizazi cha sasa.
Ziara hiyo inaongozwa na vigogo wa muziki wa Tanzania Madee Ali, Fid Q na Babu Tale, ambao wamekuwa wakiunganisha wasanii mbalimbali kusherehekea safari na maendeleo ya Bongo Flava tangu katikati ya miaka ya 1990.
Kahama itakuwa kituo cha saba cha ziara hiyo, iliyozinduliwa rasmi katika huko Mlimani City jijini Dar es Salaam Julai 2026.
Tangu kuanzishwa kwake, tamasha hiyo imefanyika katika miji sita, ambayo Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Zanzibar na Mbeya, waandalizi wakidhamiria kufikia mikoa yote.
Waandaaji wameahidi burudani ya aina yake itakayowakumbusha mashabiki nyimbo zilizotamba na kuipa Bongo Flava utambulisho wake, sambamba na vibao vipya vinavyotikisa chati za muziki.