Rais Ruto: Shilingi milioni 400 zitatumika kuboresha bandari ya Sio Port

Kiongozi wa taifa yuko kwenye ziara ya siku nne katika eneo la Magharibi mwa nchi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto akagua ukarabati wa bandari ya Sio Port kaunti ya Busia.

Rais William Ruto, amesema serikali itatumia kitita cha shilingi milioni 400, kuboresha bandari ya Sio Port katika kaunti ya Busia.

Akizungumza alipokuwa akikagua hatua zilizopigwa za kuimarisha bandari hiyo katika eneo bunge la Funyula, kiongozi wa taifa alidokeza kuwa shughuli hiyo itakapokamilika, badari hiyo itapiga jeki sekta ya uvuvi na kuboresha uchumi wa eneo hilo.

“Kwa miongo kadhaa, wakazi wa Busia wamesubiri kuimarishwa kwa bandari ya Sio Port, wakitambua uwezo wake mkubwa wa kubadilisha uchumi wa eneo hili,” alisema Rais Ruto.

Kulingana na Rais Ruto, mradi wa Sio Port ambao ulikuwa umekwama kwa muda mrefu unatarajiwa kukamilika  kufikia mwezi  Februari mwaka 2027.

“Leo tunahakikisha subira hiyo ya muda mrefu inatimia kwa kupanua bandari ya Sio port, shughuli inayotekelezwa na Halmashauri ya Bandari Nchini na Halmashauri ya Ujenzi wa Meli Nchini,” alidokeza Rais Ruto.

Kiongozi wa taifa yuko kwenye ziara ya siku nne katika eneo la Magharibi mwa nchi.

 

Share This Article