Mtihani wa KCSE kumalizika leo Ijumaa

Jumla ya watahiniwa 1,048,355 walijisajili kufanya mtihani wa KCSE mwaka huu uliosimamiwa katika vituo 10,693 nchini kote. 

Martin Mwanje
1 Min Read

Mtihani wa maandishi wa kidato cha nne, KCSE wa mwaka huu ambao umekuwa ukiendelea kwa kipindi cha takriban wiki tatu zilizopita utakamilika leo Ijumaa. 

Watahiniwa zaidi ya milioni moja walianza kufanya mtihani huo Novemba 2 huku wakikunja jamvi la msimu wa mtihani huo kwa kufanya mtihani wa kivitendo wa Fizikia.

Jumla ya watahiniwa 1,048,355 walijisajili kufanya mtihani wa KCSE mwaka huu uliosimamiwa katika vituo 10,693 nchini kote.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya mitihani ya kitaifa nchini kwa idadi hiyo ya watahiniwa kuzidi milioni moja.

Idadi hiyo inaonyesha ongezeko la asilimia 5.27 ikilinganishwa na watahiniwa 995,860 waliojisajili mwaka 2025, huku mwaka 2024 ukiwa na watahiniwa 965,172.

Msimu wa mitihani ya KCSE 2026 ulianza Oktoba 19 kwa mitihani ya maongezi, vitendo na masomo yenye watahiniwa wachache, ambayo tayari yamefanywa na watahiniwa waliojisajili kwa masomo husika.

Mitihani mikuu ya maandishi imeanza leo Jumatatu, ambapo watahiniwa walipangiwa kufanya Karatasi ya Kwanza ya Kiingereza asubuhi na Karatasi ya Kwanza ya Kemia alasiri.

Ulinzi mkali uliwekwa wakati wa kipindi cha mtihani kuhakikisha hakuna visa vya udanganyifu.

Share This Article