Thandie Malaika Wanjiku Gitao, binti mwenye umri wa miaka 18 wa mwigizaji Regina Wambui Gitao anayefahamika pia kama Regina Re, amefunguliwa mashtaka ya mauaji ya nyanya yake Dorita Lasinder Macharia, mwenye umri wa miaka 86.
Thandie hata hivyo, alikanusha kosa hilo mbele ya alikana shtaka hilo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Diana Kavedza siku ya Jumatano.
Licha ya kuwa wakili wa upande wa utetezi alifahamisha mahakama kuwa msichana huyo ana utumamu wa akili kujibu mashtaka dhidi yake, mahakama iliamuru afanyiwe uchunguzi wa afya ya akili, ripoti hiyo ikitarajiwa kuwasilishwa kwenye kikao kinachofuata cha mahakama.
Upande wa mashtaka umepinga kuachiliwa kwake kwa dhamana, ukizingatia uzito wa shtaka, hatari ya kuingilia mashahidi, na masuala ya kiusalama.
Malaika ataendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri hadi atakapofikishwa tena mahakamani tarehe 3 Desemba mwaka huu.
Upande wa mashtaka unaongozwa na naibu mkurugenzi mwandamizi wa mashtaka ya umma Gikui Gichuhi, na naibu mkurugenzi wa mashtaka ya Umma Christine Timoi.