Mtu mmoja afariki kwenye ajali ya mashua Senegal

Kulingana na maafisa wa eneo hilo, mashua hiyo iligonga mwamba kwenye bahari na kusombwa na maji hadi kwenye ufuo kutoka siku ya Jumanne hadi Jumatano.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mtu mmoja afariki kwenye ajali ya mashua Senegal.

Mashua moja iliyokuwa ikiwasafirisha wahamiaji na wakimbizi, ilipinduka katika pwani ya Yenne, Magharibi mwa Senegal na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Kulingana na maafisa wa eneo hilo, mashua hiyo iligonga mwamba kwenye bahari na kusombwa na maji hadi kwenye ufuo kutoka siku ya Jumanne hadi Jumatano.

Manusura mmoja aliyehojiwa, alisema wakati wa mkasa huo, mashua hiyo ilikuwa na takriban watu 100, waliojumuisha wanawake watano

Meya wa eneo la Yenne Massamba Mbengue pamoja na wazima moto, walisema mwili mmoja ulipatikana baada ya ajali hiyo.

Oumar Sow, mwakilishi wa chifu wa eneo hilo, alisema ajali hiyo ilitokea saa nane usiku saa za eneo hilo.

Ajali hiyo inajiri siku kumi baada ya mashua nyingine kuzama na kusababisha vifo vya watu 43, ajali iliyotajwa mbaya zaidi katika hisoria ya taifa hilo.

TAGGED:
Share This Article