Timu ya AS FAR kutoka Morocco ilifanikiwa kuhifadhi tajila Ligi ya Mabingwa kwa wanawake barani Afrika, kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mamelodi Sundowns kwenye fainali Jumapili jioni mjini Ismailia, Misri.
Imane Touriss alitikisa nyavu mara mbili naye Hiba Youssifi akaongeza jingine wakati Mamelodi ya kutoka Afrika Kusini ikijipatia bao la kufutia machozi kupitia kwa Refilwe Tholakele.
AS FAR waliandikisha historia kuwa timu ya kwanza kutwaa kombe hilo mara tatu na kuzawadiwa dola laki sita.
Timu hiyo ya Rabat ilitwaa ubingwa huo mwaka 2022, 2025 na sasa mwaka 2026.
Fainali hiyo ilikuwa marudio ya fainali ya mwaka 2022, wakati Sundowns waliibwaga AS FAR mabao 4-0 mjini Rabat na kushinda kombe la kwanza.
Kando na ushindi, AS FAR wamefuzu kwa raundi ya pili kombe la wanawake duniani mwaka 2027.