Serikali ya Uganda imetangaza kurejelea usafiri wa treni za abiria kati ya miji ya Kampala na Jinja,takriban miongo mitatu tangu kusitishwa kwa huduma hizo.
Shirika la Reli la Uganda (URC) limesema mchakato wa kurejelea usafiri huo zipo katika hatua ya mwisho.
Aidha,URC imeongeza kuwa kufunguliwa kwa treni hizo kutapunguza msongamano wa magari pakubwa huku taifa hilo likijiandaa kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 kwa ushirikiano na Kenya na Tanzania.
Huduma hizo zilisitishwa mapema miaka ya 90 baada ya URC kupitia changamoto za kiufundi na uhaba wa pesa.