Emerging Stars yaabiri ndege kwenda Abidjan

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 23,Emerging Stars, imeondoka mapema Jumamosi kuelekea Abidjan,Ivory Coast kwa mechi ya marudio raundi ya pili kufuzu kwa fainali za AFCON.

Kenya inayofunzwa na kocha Anthony Kimani, italenga kudumisha uongozi wa mabao  2-1, kutokana na mkumbo wa kwanza wiki jana jijini Nairobi .

Ivory Coast itawaalika Kenya Jumanne  usiku huku mshindi wa jumla akijikatia tiketi kwa fainali za mwaka ujao za mataifa ya Afrika ambazo pia zitatumika kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028.

Timu nane ikiwemo wenyeji Misri zitashiriki fainali za mwaka ujao za AFCON.

Share This Article