Mkutano wa wajumbe wa Linda Mwananchi kufanyika faraghani leo

Taarifa kutoka kwa kitengo cha masiliano cha muda cha LLM kikiongozwa  Pauline Njoroge,  IIisema kuwa  wanahabari wala watu wasio wajumbe hawataruhusiwa kuingia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkutano wa wajumbe wa vuguvugu la Linda Mwanchi  (LLM) unaotarajiwa kufanyika leo Ijumaa Novemba 13, utaandaliwa faraghani .

Taarifa kutoka kwa kitengo cha masiliano cha muda cha LLM kikiongozwa  Pauline Njoroge,  IIisema kuwa  wanahabari wala watu wasio wajumbe hawataruhusiwa kuingia.

Aidha,eneo la kuandaliwa kwa mkutano hao bado halijawekwa wazi na kuibua maswali mengi.

Mkutano huo unaotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa muungano huo akiwemo  Edwin Sifuna  anayepigiwa upato kupokezwa bendera huenda ukaweka bayana maswala kadhaa ya uongozi kabla ya Sifuna kuanza ziara ya wiki  mbili nchini Marekani kuanzia wiki ijayo kutafuta uungwaji mkono.

 

Share This Article