Idadi ya walioambukizwa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na visuri aina ya Bundiburgyo katika Jamhuri Kidemokrasia ya Congo (DRC) imefika 11,000.
Hii ni kulingana na takwimu zilizotolewa na serikali.
Takwimu hizo zilizotolewa siku ya Jumatano zinaashiria kuwa watu 5,387 wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa huo.
Serikali imetoa takwimu hizo, huku ikijizatiti kukabiliana na msambao wa ugonjwa huo ambao umetajwa kuwa mbaya zaidi katika historia ya DRC.
Mikoa minane kati ya 26 imeathriwa na ugonjwa huo, huku vifo vingi vikiripotiwa nje ya vituo vya matibabu.
Ukosefu wa kugundua ugonjwa huo mapema, huduma duni za afya na ghasia katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo, ni baadhi ya masuala yanayodumaza juhudi za kutokomeza ugonjwa huo na kuufanya kuenea zaidi ikilinganishwa na milipuko ya ugonjwa ya hapo awali.
Barani Afrika, Ebola imewaangamiza watu zaidi ya 15,000 katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.