Miamba wa Uingereza Manchester United wameafikia kumteua Mauricio Pochettino kuwa meneja kumrithi Michael Carrick.
Yamkini uamuzi huo uliafikiwa jana Jumatano baada ya kikao kilichoandaliwa mjini Monaco, Ufaransa.
Hata hivyo, The Red Devils Man watalazimika kuilipa timu ya taifa ya Marekani pauni milioni 7, ili Pochettino aruhusiwe kuondoka, kulingana na mkataba aliousaini na timu ya Marekani punde baada ya fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.
Carrick aliongoza mazoezi ya United Jumatano huku duru zikiarifu kuwa huenda apigwe shoka kabla ya mwishoni mwa juma hili.