Mtu mmoja amefariki na wengine wawili kujeruhiwa baada ya ndovu kuwashambulia wakazi wa eneo la Kabote, kaunti ya Tharaka Nithi.
Shambulizi hilo la ndovu hao wanaoaminika kutoka Mbuga ya Kitaifa ya Meru, limeibua upya wasiwasi kuhusu mzozo kati ya binadamu na wanyamapori katika eneo hilo.
Afisa Mkuu wa Shirika la Huduma kwa Wanyamapori (KWS) kaunti ya Tharaka Nithi Caleb Mumanyi, amwaonya wakazi dhidi ya kuwakaribia wanyama hao au kujaribu kuwapiga picha kwa karibu, akisema hatua hiyo inahatarisha maisha yao.
Aidha, Mumanyi ametoa wito kwa wakazi kuripoti mara moja punde tu wanapowaona wanyamapori, ili kufanikisha juhudi za mapema kutoka kwa shirika la KWS kuzuia mashambulizi.
Akithibitisha kifo hicho, Naibu wa Chifu wa eneo la Matakiri Festus Kirema, alisema visa vya wanyamapori kutoroka kwenye mbuga vimeongezeka katika siku za hivi karibuni.