Rais Ruto awateua maafisa wakuu 5 wa mashirika ya serikali

Wakati huo huo, kiongozi wa taifa alimteua Lydia Sitienei Chelagat kuwa Kamishna wa Data, akisubiri kuidhinishwa na bunge.

Tom Mathinji
1 Min Read
William Ruto - Rais wa Kenya.

Rais William Ruto, amewateua Maafisa Watendaji Wakuu katika mashirika 5 ya serikali,  hatua inayolenga kuimarisha utenda kazi na utoaji huduma wa mashirika hayo.

Kupitia kwa taarifa Jumatatu jioni, Waweru Karanja ameteuliwa kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa  Halmashauri ya Ubinafsishaji, huku Wakhungu Patrick Murunga akichukua wadhifa sawia na huo katika Taasisi ya Kanda kuhusu Elimu ya maji ya chini ya ardhi, mafunzo na utafiti Afrika Mashariki  (RCGW).

Peninah Wangare Wahome, ameteuliwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Halmashauri ya Kupambana na dawa za kusisimua misuli (ADAK), naye John Washington Agutu akiteuliwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Kitaifa la Nyumba. Dkt. Janerose Omondi atachukuwa wadhifa wa kaimu Afisa mkuu Mtendaji wa Hazina ya kitaifa ya uwekezaji wa ujasiriamali (KNEST).

Wakati huo huo, kiongozi wa taifa alimteua Lydia Sitienei Chelagat kuwa Kamishna wa deta, akisubiri kuidhinishwa na bunge.

Msemaji wa serikali Charles Owino Wahong’o, alidokeza kuwa uteuzi wa maafisa hao ulitekelezwa na bodi husika za usimamizi kupitia mchakato wenye ushindani mkali wa uajiri.

Share This Article