Karauri atua UDA,kuwania ugavana Nairobi

Karauri atakabilina na Johnson Sakaja kuwania Ugavana wa Nairobi katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mbunge wa Kasarani Ronald Karauri  amejiunga rasmi na chama cha United Democratic Movement (UDA) huku akitangaza azma ya kuwania Ugavana wa  gatuzi la Nairobi.

Karauri aliyechaguliwa bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2022 akiwa mwaniaji huru, alikaribishwa rasmi katika chama cha UDA siku ya Jumatatu katika makao makuu ya chama hicho na Katibu Mkuu Hassan Omar Hassan.

Kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichung’wah alikuwa miongoni mwa Wabunge  waliomkaribisha Karauri katika chama  cha UDA.

Karauri atakabilina na Johnson Sakaja wa ODM kuwania Ugavana wa Nairobi katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

 

Share This Article