Kanu na Wanyama kukutana katika mechi ya magwiji uwanjani Nyayo Ijumaa

Kando na mechi hiyo magjwi hao wa Arsenal wataandaa kliniki ya wakufunzi Jumamosi Novemba 14 katika shule ya Crawford International School.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshambulizi wa zamani wa Nigeria  Nwankwo  Kanu atawaongoza magwiji wengine wa klabu  ya Arsenal  kwa mchuano wa kirafiki dhidi ya Harambee Stars Ijumaa hii Novemba 13, katika uwanja wa Nyayo.

Kanu aliye na umri wa miaka 50 ataongoza  magwiji wengine wa Arsenal wakiwemo Bacary Sagna, Gervinho, Alex Song, Yaya Sanogo, Tony Adams, Robert Pirès, Ashley Cole, Gilberto Silva, Santi Cazorla, na  Theo Walcott.

Victor Wanyama ataongoza kikosi cha magwiji Harambee Stars kinachojumuisha  McDonald Mariga, Dennis Oliech, John Bobby Ogolla, Francis Kahata, Francis Onyiso, Jamal Mohammed, JJ Masiga, na Mahmoud Abbas.

Pambano  hilo litapigwa uwanjani Nyayo kuanzia saa moja usiku .

Kando na mechi hiyo magjwi hao wa Arsenal wataandaa kliniki ya wakufunzi Jumamosi Novemba 14 katika shule ya Crawford International School.

Share This Article