Nyumba zaidi ya 5,000 kuunganishwa umeme eneo bunge la Bomachoge Borabu

Martin Mwanje
1 Min Read

Wakazi wa eneo bunge la Bomachoge Borabu katika kaunti ya Kisii wana kila sababu ya kutabasamu kwani huenda wasitafunwe tena na giza totoro la usiku kucha hivi karibuni. 

Hii ni baada ya Rais William Ruto kutangaza kuwa nyumba zaidi ya 5,000 eneo hilo zitaunganishwa umeme.

“Tunawekeza shilingi milioni 330 ili kuunganisha umeme kwa nyumba 5,400 katika eneo bunge la Bomachoge Borabu, kaunti ya Kisii,” alisema Rais Ruto.

Aliyasema hayo leo Jumatatu wakati akizindua mradi wa Last Mile Electricity Connectivity wa kuunganisha umeme kwa nyumba 180 katika wadi ya Boochi Borabu.

Share This Article