Ruto aanza ziara ya siku nne kaunti za Kisii na Nyamira

Kiwango kingine cha shilingi nusu bilion kitatumika kuunganisha umeme kwa nyumba 6,480 katika kaunti hiyo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Jumapili ameanza ziara yake ya siku nne katika kaunti za Nyamira na Kisii, akiwatahadhari wakazi wa eneo hilo kutocheza karata na kura zao mwaka ujao.

Akiwa katika soko la Nyabite, West Mugirango kaunti ya Nyamira,Rais amewasuta wapinzani wake, akisema hawana ajenda yoyote na suluhu kwa changamoto zinazokabili taifa .

Ruto amesisitiza kuwa serikali jumuishi ya chama cha UDA na ODM inalenga kuwaunganisha Wakenya wote bila kuzingatia misingi ya kikabila.

Rais ameusuta muungano wa upinzani akitaja kuwa hauna mwelekeo na kukosa ajenda ya taifa kuelekea kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Aliwaahidi wakazi wa kaunti ya Nyamira kuwa serikali yake imetenga shilingi bilioni 11 kwa uwekaji lami barabaraba za umbali wa kilomita 180 .

Ruto aliongeza kuwa shilingi nyingine bilioni 10 zimetengwa kwa minaajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu,masoko ya kisasa na mabweni ya wanafunzi.

Kiwango kingine cha shilingi nusu bilion kitatumika kuunganisha umeme kwa nyumba 6,480 katika kaunti hiyo.

Akiwa Nyamira Rais pia amezindua kituo cha teknolojia ya Habari na mawasiliano katika eneo bunge la South Mugirango,kando na kuhudhuria ibada iliyoshirikisha madhehebu mbalimbali katika uwanja wa Nyamaiya eneo bunge la West Mugirango.

Share This Article