Kenya Lionesses wafungua mashindano ya Raga Afrika kwa ushindi

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wanawake saba kila upande maarufu Lionesses, imeanza mashindano ya kuwania kombe la Afrika kwa ushindi wa pointi  27-7 dhidi ya Ghana.

Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa RFEUA Jijini Nairobi Jumamosi jioni, imeshuhudia Kenya wakipata ushindi kwa njia rahisi  katika kundi B.

Mashindano hayo ya siku mbili yanajumuisha timu 11 huku mabingwa wakifuzu kwa mashindano ya msururu wa dunia divisheni ya tatu mwaka ujao.

 

Share This Article