Polisi wanasa mihadarati Bungoma na Busia

Mihadarati hiyo ilikuwa yenye uzani wa kilo 170.8 na inakisiwa kuwa ta thamani ya shilingi 5,124,000.

Tom Mathinji
1 Min Read
Polisi wanasa mihadarati Bungoma na Busia.

Maafisa wa Polisi wameimarisha vita dhidi ya ulanguzi wa mihadarati, huku wakinasa bidhaa zinazoshukiwa kuwa dawa za kulevywa katika kaunti ya Bungoma na Busia.

Baada ya kupokea habari za kijasusi, Maafisa wa Polisi katika kaunti ya Bungoma walisimamisha gari kwenye Barabara Kuu ya Malaba–Webuye, na baada ya kulipekua walipata mifuko 162 inayoshukiwa kuwa mihadarati. Waliokuwa kwenye gari hilo walitoroka.

Mihadarati hiyo ilikuwa yenye uzani wa kilo 170.8 na inakisiwa kuwa ta thamani ya shilingi 5,124,000.

Katika kaunti ya Busia, maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria katika barabara ya Bundokomi–Mundika, walisimamisha pikipiki iliyokuwa imebeba magunia ya kijani kibichi, na baada ya kulipekua walipata bidhaa zinazoshukiwa kuwa bangi.

Aliyekuwa akiendesha pikipiki hiyo alitoroka, huku polisi wakilipeleka pamoja na mihadarati hiyo katika kituo cha polisi.

Huduma ya Taifa ya polisi imeelezea kujitolea kwake kukabiliana na ulanguzi wa mihadarati kote nchini, ikipongeza umma kwa kutoa habari kuhusu shughuli za ulanguzi wa mihadarati.

Share This Article