Sheila Chepkirui atwaa ubingwa wa New York Marathon,Obiri amaliza wa tatu

Chepkirui sasa ana mataji mawili ya mbio hizo sawia na Obiri baada ya kushinda mwaka 2024, kwa mara ya kwanza kabla kumpisha Obiri ambaye awali alikuwa amenyakua ushindi mwaka 2023.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkenya Sheila Chepkirui amenyakua taji ya pili ya mbio za New York City Marathon nchini Marekani Jumapili jioni baada ya kukata utepe kwa muda wa saa 2 dakika 24 na 36.

Jess McClain wa Marekani amemaliza wa pili kwa saa 2 dakika 24 na sekunde 42 sekunde moja nyuma ya bingwa mtetezi Hellen Obiri wa Kenya aliyemaliza nafasi ya tatu.

Edna Kiplagat na Mercy Chelangat walimaliza katika nafasi za nne na tano mtawalia.

Chepkirui sasa ana mataji mawili ya mbio hizo sawia na Obiri baada ya kushinda mwaka 2024, kwa mara ya kwanza kabla kumpisha Obiri ambaye awali alikuwa amenyakua ushindi mwaka 2023.

Andreas Almgren wa Uswidi alitawazwa bingwa wa mbio za wanaume kwa kutumia saa 2 dakika 6 na sekunde 1,sekunde 13, mbele ya Mwitaliano Yemaneberhan Crippa,huku Kamohelo Mofolo wa Lesotho akikamilisha tatu bora.

Bingwa mtetezi Benson Kipruto alichukua nafasi ya nne kwa muda wa saa 2 dakika na sekunde 27,sekunde moja nyuma ya Mofolo.

Share This Article