Klabu ya Voliboli ya wanawake ya Kenya Commercial Banka,(KCB), imewasajili wachezaji watatu wapya kuimarisha kikosi chake kwa msimu mpya wa Ligi Kuu wa mwaka 2026/2027.
KCB imewasa wachezaji hao watatu akiwemo kiungo Juliet Naliaka Wakwabubi,mshambulizi Christene Gati na mlinzi Ruth Atabo, wote kutoka kwa Akademia ya shule ya Kesogon Senior.
Klabu hiyo pia imemsajili Msham,bulizi wa pembeni Mercy Cherono kutoka klabu ya Kenya Prisons.
Ligi kuu hiyo itakayoshirikisha vlabu 16 vya wanaume na kumi vya wanawake itango’a nanga kati ya Novemba 14 na 15.
KCB inalenga kuboresha matokeo ya msimu jana ilikomaliza ya tatu katika Ligi Kuu ,baada ya kupoteza seti 2-3, dhidi ya Kenya Pipeline, katika fainali iliyoandaliwa ukumbini Kasarani mwezi Julai mwaka huu.