Timu ya Kenya kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 17, iliweka historia kwa kucheza hadi raundi ya 16 bora katika fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Morocco.
Junior Starlets ya Kenya ilifuzu kwa raundi ya 16 kwa mara ya kwanza kufuatia ushindi wa ma mabao 4-0 dhidi ya Samoa, katika mechi ya mwisho ya kundi E.

Historia ya Kenya ni baadhi ya sehemu ya ufanisi wa Morocco kuandaa mashindano ya haiba kuu ambapo wachezaji wamepata fursa ya kudhihirisha vipaji.
Afrika iliwakilishwa na timu tano zikiwemo Zambia,Kenya,Nigeria,Ghana na wenyeji Morocco.
Fainali hizo zinashirikisha mataifa 24 ambayo kwa pamoja yatacheza jumla ya mechi 52 kushindania ubingwa.

Mechi hizo zimekuwa zikiandaliwa katika uwanja wa michezo wa Mohammed 6 jijini Rabat.
Kwa sasa bara lote la Afrika linajizatiti kugeuza ufanisi wa maandalizi kwa ukuzaji talanta wa muda mrefu.

Haya yanajumuisha maendeleo ya wachezaji,kuimarisha vlabu,kukuza timu za taifa za wanawake na kukuza mashindano ya timu za taifa ili kudumisha viwango vilivyowekwa na Morocco kuwa viwango vya bara Afrika.