Kenya yanyofolewa na Marekani,Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read
Screenshot

Timu ya Kenya ya wanawake chini ya umri wa miaka 17,iliambulia kichapo cha kitutu  cha mabao 6-1 na Marekani katika macho ya pili ya kundi E kuwania Kombe la Dunia.

Pambano hilo lililoskatwa katika uchanjaa wa Mohammed 6,jijini Rabat,Morocco lilishuhudia Marekani wakiongoza magoli 4-0 kufikia mapumzikoni.

Maddie DiMaria alipachika magoli manne ya Marekani dakika za 2,22,35 na dakika ya pili ya muda wa mazidadi.

Loradana Paletta alifunga bao la tano dakika tatu ndani ya kipindi cha pili naye nguvu mpya Hanif Gianni akaongeza jingine dakika ya 93.

Lindey Atieno alifunga goli la kufutia machozi kwa Kenya dakika ya 96.

Kenya watarejea watarejea uwanjani Jumapili hii dhidi ya Samoa, katika mchuano ambao vipusa hao wa kocha Mildred Cheche ni sharti washinde kwa mabao mengi ili kuwa na fursa ya kufuzu kwa raundi ya 16 bora.

Share This Article