Kenya yaagiza chanjo 10,000 za Ebola

Haya yanajiri huku Kenya ikiripoti visa tisa vya maambukizi ya Ebola ikiwemo kifo kimoja.

Dismas Otuke
1 Min Read
Screenshot

Kenya imeagiza chanjo 10,000 za kuzuia maambukizi ya  ugonjwa wa Ebola zitakazopewa wahudumu wa afya.

Mkurugenzi mkuu wa Afya Patrick Amoth amesema Kenya tayari imezungumza na shirika la afya ulimwenguni (WHO) na vituo vya Afrika vya kuzuia magonjwa ili kupewa chanjo hiyo.

Kenya imeagiza chanjo ya Everbo inayofanyiwa majaribio kuzuia virusi vya Bundibugyo vinavyosababisha ugonjwa wa Ebola.

Haya yanajiri huku Kenya ikiripoti visa tisa vya maambukizi ya Ebola ikiwemo kifo kimoja.

Share This Article