Ruto: Afrika inapaswa kuimarisha taasisi zake za kifedha

Alitoa wito kwa serikali za Afrika kuwekeza zaidi kwenye taasisi za bara hili, huku akizitaka zitekeleze miradi ya maendeleo na taasisi hizo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto akihutubia mkutano wa COMESA, Jijini Harare Zimbabwe.

Rais William Ruto ametoa wito kwa bara Afrika kufadhili miradi yake ya maendeleo, kwa kuimarisha taasisi zake za kifedha.

Alizitaka nchi za Afrika kuwa na imani na taasisi zake, akisema tayari zimeonyesha uwezo mkubwa hasaa katika kufadhili biashara barani Afrika, na zimesimama na mataifa ya Afrika hata nyakati za hali ngumu.

Alitoa wito kwa serikali za Afrika kuwekeza zaidi kwenye taasisi za bara hili, huku akizitaka zitekeleze miradi ya maendeleo na taasisi hizo.

“Hatuwezi himiza ulimwengu uwe na imani na taasisi za Afrika, ikiwa sisi hatuna imani nazo. Afrika ina rasilimali ya takriban dola trilioni 4. Lakini nyingi ya rasilimali hizo ziko katika nchi za kigeni,” alisema Rais Ruto.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo siku ya Alhamisi, wakati wa mkutano wa 25 wa viongozi wa nchi na serikali wa  Soko la Pamoja la Kusini na Mashariki mwa Afrika (COMESA), ulioandaliwa Jijini Harare, Zimbwabwe.

Share This Article