DRC yaripoti Ebola katika mkoa wa nane mpakani na Afrika ya Kati

DRC imeripoti jumla ya maambukizi 9,415 na vifo 4,536 ya Ebola  tangu  ugonjwa  huo kutangazwa kuzuka  nchini humo mwaka mmoja uliopita.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeripoti virusi vya Ebola katika mkoa wa nane, huku idadi ya maambukizi na vifo ikipanda kila kuchao.

Kulingana na taasisi ya afya nchini humo  virusi vya Bundiburgyo vinavyosababisha Ebola, vimeripotiwa katika mkoa wa Ubangi Kaskazini,katika mpaka wa DRC na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Mamlaka ya afya imesema visa viwili vya Ebola vimeripotiwa kikiwemo kifo kimoja katika mkoa huo.

Ubangi Kaskazini unajiunga na mikoa mingine saba iliyo na maambukizi ya Ebola nchini DRC ikiwemo;-Kivu Kaskazini,Ituri,Haute Uele,Tshopo,Sud Kivu,Bas Uele na Kivu Kusini.

DRC imeripoti jumla ya maambukizi 9,415 na vifo 4,536 ya Ebola  tangu  ugonjwa  huo kutangazwa kuzuka  nchini humo mwaka mmoja uliopita.

 

Share This Article