Nigeria yathibitisha kisa cha kwanza cha Ebola

Habari za awali zinaashiria kuwa mwathiriwa huyo alisafri kupitia Uganda mapema mwezi Oktoba bila dalili za ugonjwa huo, lakini akapata dalili za Ebola alipowasili Nigeria.

Tom Mathinji
1 Min Read
Nigeria yathibitisha kisa cha kwanza cha Ebola.

Wizara ya Afya ya Nigeria, imethibitisha kisa cha kwanza cha maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, kinachomhusisha mwanamke aliyesafiri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa shughuli za kibiashara.

Habari za awali zinaashiria kuwa mwathiriwa huyo alisafri kupitia Uganda mapema mwezi Oktoba bila dalili za ugonjwa huo, lakini akapata dalili za Ebola alipowasili Nigeria.

Serikali ya Nigeria bado haijatoa ratiba kamili ya safari ya mwathiriwa huyo na historia yake ya matibabu ambayo itasaidia kwa uchunguzi zaidi, na kufanikisha shughuli za kuwafuatilia waliotangamana naye.

“Tungependa kufafanua kwamba, hadi wakati wa kutoa taarifa hii, Uganda haina kisa chochote cha ugonjwa wa Ebola,” ilisema taarifa ya wizara hiyo.

Wizara hiyo ilisema kwa ushirikiano na asasi zingine husika, itaimarisha uchunguzi wa ugonjwa huo katika maeneo ya kuingia nchini humo.

Hata hivyo, imetoa wito wa utulivu, kuwa makini na uzingatiaji wa hali ya juu ya usafi, ikidokeza kuwa itaendelea kutoa habari zilizothibitishwa kupitia mifumo rasmi.

Share This Article