Mahakama ya CAS kuamua mabingwa wa AFCON mwaka 2025 ,mwezi ujao

CAS imesema kesi hiyo iliskizwa kisiri tarehe 8 mwezi huu,na jopo limeanza kuandaa uamuzi .

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama ya kimataifa ya kutatua migogoro michezoni (CAS) imesema itatoa uamuzi wake kuhusu ni timu ipi kati ya Morocco na Senegal ilinyakua Kombe la mataifa ya Afrika mwaka jana ,kufikia mwishoni mwa mwezi ujao.

Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari CAS yenye makao yake mjini Laussane ,Uswizi, kesi hiyo itachukua muda kuskiza pande zote kabla ya kutoa uamuzi wa mara moja.

Shirikisho la soka nchini Senegal (FSF)  lilikuwa limeshtaki Shirikisho la soka Afrika (CAF) pamoja na shirikisho la kandanda nchini Morocco (FRMF) baada ya CAF kutangaza Morocco kuwa mabingwa wa AFCON.

CAS imesema kesi hiyo iliskizwa kisiri tarehe 8 mwezi huu,na jopo limeanza kuandaa uamuzi .

Waendesha mashtaka wa mahakama hiyo wameamua kutoa uamuzi wa pamoja  kwa kuzingatia misingi yote ya kesi hivyo itahitaji muda zaidi  huku uamuzi wa mwisho ukitarajiwa kufikia mwisho wa mwezi Novemba mwaka huu.

Share This Article