Papa Leo XIV, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe mdogo kwenye mapafu yake.
Leo mwenye umri wa miaka 71, alielezea kuhusu ugunduzi wa uvimbe huo mdogo wakati wa sala yake ya Jumapili adhuhuri na kutangaza kwamba anataka uondolewe.
Hata hivyo matabibu wanasema kuwa upasuaji huo utaamua iwapo uvimbe huo utatolewa ama aina nyingine ya matibabu itatumika.
Upasuaji huo utatekelezwa katika ospitali ya kifahari ya Gemelli hospital, ambayo imekuwa ikiwatibu viongozi hao wa kanisa katoliki kwa miongo kadhaa.
Kulingana na mamlaka ya Vatican, Papa Leo XIV alitarajiwa kulazwa leo Jumanne, lakini haikuelezea saa za upasuaji huo.
Teknolojia ya roboti pia huenda ikatumika kwenye uchunguzi wa uvimbe huo kabla ya upasuaji kutekelezwa.