Muthomi Njuki achaguliwa Mwenyekiti wa Baraza la Magavana

Uchaguzi wa wawili hao umefanyika leo Jumatatu katika kikao kilichohudhuriwa na Magavana wote katika hoteli moja jijini Nairobi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki ndiye Mwenyekiti mpya wa Baraza la Magavana nchini (CoG). 

Atahudumu kwa kipindi cha miaka miwili akisaidiwa na Gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka.

Njuki anatwaa naafsi ya Gavana wa Wajir Ahmed Abdullahi, ambaye amekuwa usukukani tangu mwaka 2024.

Uchaguzi wa wawili hao umefanyika leo Jumatatu katika kikao kilichohudhuriwa na Magavana wote katika hoteli moja jijini Nairobi.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Njuki alikubali uteuzi huo akiahidi kuwa CoG itaendelea kupigania kuongozwa kwa mgao wa fedha kwa kaunti.

Aidha, alisema baraza hilo litapigania kutengewa shilingi nusu bilioni mwaka 2027 ili kuhakikisha kaunti zinatekeleza majukumu yake ipasavyo.

Njuki aliongeza  kuwa changamoto kubwa ya CoG ni uhaba wa pesa, akiahidi kuwashirikisha wadau wa kibinafsi na kutoka kwa mashirika ya serikali ili kupata suluhu.

Share This Article