Brigid Kosgei na Amos Kipruto kuwaongoza Wakenya Chicago marathon Jumapili

Kosgei atamenyana na bingwa wa mwaka huu wa mbio za Boston Marathon Sharon Lokedi,Briallian Kipkoech,Loice Chemnung,Joan Kilimo,Magdalene Maasai na Mary Ngugi Cooper.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia  Brigid Kosgei na Amos Kipruto aliyemaliza wa pili mwaka jana watarejea kutimika makala ya mwaka huu ya mbio za Chicago Marathon nchini Marekani Jumapili  jioni.

Kosgei atamenyana na bingwa wa mwaka huu wa mbio za Boston Marathon Sharon Lokedi,Briallian Kipkoech,Loice Chemnung,Joan Kilimo,Magdalene Maasai na Mary Ngugi Cooper.

Ushindani unatarajiwa kutoka kwa bingwa mtetezi Hawi Feysa wa Ethiopia.

Kipruto atatimka mbio za wanaume akishirikiana na Daniel Mateiko huku wakipata ukinzani kutoka kwa bingwa mtetezi Jacob Kiplimo wa Uganda na Waethiopia Milkesa Mengesha na Tadese Takele Bikila.

Share This Article