Marekani kununua mafuta ya diesel kutoka Urusi

Kulingana na Trump, rais wa Urusi Vladimir Putin amekubali kuiuzia Marekani tani 300,000 za dizeli.

Tom Mathinji
1 Min Read
Marekani kununua diesel kutoka Urusi.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa Marekani itaagiza mafuta ya diesel kutoka Urusi, wakati ambapo anakabiliwa na shinikizo kupunguza bei za mafuta nchini humo.

Kulingana na Trump, rais wa Urusi Vladimir Putin amekubali kuiuzia Marekani tani 300,000 za dizeli pamoja na soko la kimataifa ikifuatiwa na tani nusu Milioni mwezi Novemba na tani nyingine Milioni moja baadaye.

Putin alisema Urusi ambayo ilianzisha marufuku kuhusiana na uuzaji wa dizeli nje ya nchi hiyo mapema mwaka huu, ilikuwa tayari kuiuzia Marekani pamoja na masoko ya kimataifa mafuta pamoja na bidhaa za petroli, lakini kauli yake haikubainisha viwango vya bidhaa hizo.

Hatua hiyo mnamo Ijumaa iliibua ghadhabu kutoka kwa rais wa Ukraine Volodymr Zelensky, ambaye alitoa kejeli akisema hiyo ni zawadi kwa Putin na sawa na uwekezaji katika vita ambavyo vinapaswa kusitishwa na wala si kuendelezwa.

Share This Article