Jumla ya watu 28 wameaga dunia nchini Tanzania baada ya basi la abiria kugongana na gari la mizigo na kisha kuwaka moto.
Joseph Mwasabeja ni Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Morogoro.
Kwenye taarifa, amesena ajali hiyo ilitokea eneo la Mkambarani mkoani humo usiku wa kuamkia leo Ijumaa.
Basi lilikuwa likitokea mjini Dar es Salaam kuelekea mkoani Mbeya wakati na lori likiwa limepakia miti.
Dereva wa lori amelaumiwa kwa kusababisha ajali hiyo kwani aliyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari eneo lisiloruhusiwa.
Majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Morogoro wanakotibiwa.