Kenya itaendelea kuandaa mashindano ya mbio za magari ulimwenguni, WRC Safari Rallly mwakani.
Kenya ilikuwa imesaini mkataba wa miaka mitano mwaka 2020 kuandaa mashindano ya mwaka 2021 hadi 2026.
Rais William Ruto amesema ni fahari kwa Kenya kuendelea kuandaa mashindano hayo baada ya WRC kuongeza mkataba.
Kenya itaandaa mkondo wa tatu wa mwaka ujao baina ya Machi 18 na 21 mjini Naivasha.
Mashindano ya Kenya yatatanguliwa na yale ya Rally Monte Carlo huko Monaco kati ya Januari 21 na 24, yakifuatwa na mkondo wa pili wa Rally Sweden baina ya Februari 18 na 21.
Mashindano ya mwaka ujao ya mbio za magari yatakuwa na mikondo 15 katika mabara matano tofauti.