Kenya yasaini makubaliano ya kutengeneza magari ya umeme

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto jana Jumanne alisimamia hafla ya kutiwa saini kwa Mkataba wa Maelewano (MoU) wa kima cha shilingi bilioni 389 ambazo ni sawa na dola bilioni 3 wa utengenezaji wa magari ya umeme nchini.

Mkataba huo ulitiwa saini kati ya serikali na shirika la Endelevu Enterprise Corporation katika Ikulu ya Nairobi.

Mradi huo utahusisha utengenezaji na ukusanyaji wa magari ya umeme wakati ukilenga kupiga jeki utengenezaji na ukusanyaji wa magari hayo humu nchini.

Akizungumza baada ya hafla ya utiaji saini makubaliano hayo, Rais Ruto alisema uwekezaji huo utaisaidia Kenya kukoma kuagiza ajira kwa kuwacha kuagiza magari ambayo tayari yametengenezwa kwa kuyaongeza thamani nchini.

Aliongeza kuwa MoU hiyo inatoa mpangokazi wa moja ya uwekezaji mkubwa wa magari ya umeme katika kanda hii.

Mpango huo unajumuisha kiwanda cha kukusanya magari 50,000 aina ya four-wheel drive kwa mwaka huku kingine kikikusanya magari 100,000 aina ya two-wheel drive miongoni mwa uwekezaji mwingine.

Share This Article