Kenya imejitolea kukabiliana na ulaji muku michezoni, asema Mvurya

Mvurya amesema hayo leo Jumatatu alipokutakana na Rais wa Shirika la Kukabiliana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli (WADA) Witold Bańka, aliye nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Michezo Salim Mvurya amekariri kujitolea kwa serikali ya Kenya kukabiliana na tatizo sugu la ulaji muku michezoni humu nchini.

Mvurya amesema hayo leo Jumatatu alipokutakana na Rais wa Shirika la Kukabiliana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli (WADA) Witold Bańka, aliye nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Aliongeza kuwa Kenya itaendelea kuongeza idadi ya vipimo wanavyofanyiwa wanariadha, elimu na hamasisho kuhusu ulaji muku, upigaji marufuku kwa wanaopatikana na hatia na uchunguzi wa kijasusi ili kubaini watumizi wa dawa hizo haramu.

Kulingana na Mvurya, serikali ya Kenya inaunga mkono ushindani michezoni usiohusisha matumizi ya dawa za kuongeza nguvu, uadlifu na kulinda hadhi ya taifa michezoni.

Witold anaandamana na kinara wa WADA Afrika Rodney Swigelaar huku akizuru Kenya kwa mara ya kwanza.

Share This Article