Mkurugenzi wa Mashindano ya Shirikisho la Riadha Duniani azuru Kenya

Kenya ilitwikwa jukumu la kuwa mwenyeji wa mashindano ya Riadha Duniani mwaka 2029 kwa mara ya kwanza ikishinda miji ya London, Uingereza na Roma, Italia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkurugenzi wa Mashindano ya Shirikisho la Riadha Duniani Pierce O’Callaghan alifanya ukaguzi wa viwanja vya kufanyia mazoezi na uwanja wa Kasarani, vitakavyotumika kwa mashindano ya Riadha Duniani mwaka 2029.

O’Callaghan alianza ziara yake siku ya Jumatano kwa kuzuru uwanja wa Kasarani ambao utaandaa mashindano hayo ya Dunia, akiandamana na maafisa kutoka Wizara ya Michezo na wale wa Chama cha Riadha Kenya.

Jana Alhamisi, alikagua viwanja vya Nyayo na Ulinzi Sports Complex ambavyo vitatumika kwa mazoezi ya wanariadha.

Baadaye, alikutana na Katibu katika Wizara ya Michezo Elijah Mwangi aliyetoa hakikisho la kujitolea kwa Kenya kuandaa mashindano ya kufana mwaka 2029.

Shirikisho la Riadha Duniani litatoa mwongozo wa jinsi ukarabati wa viwanja na miundombinu mingine unavyostahili kufanywa ili kuafiki viwango vya kimataifa.

Kenya ilitwikwa jukumu la kuwa mwenyeji wa mashindano ya Riadha Duniani mwaka 2029 kwa mara ya kwanza ikishinda miji ya London, Uingereza na Roma, Italia.

Share This Article