Timu ya taifa ya Kenya kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 23, itawaalika Tanzania katika mkondo wa kwanza wa mechi ya mchujo kufuzu fainali za kombe la bara Afrika, AFCON.
Pambano hilo litasakatwa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo kuanzia saa tisa alasiri.
Mechi ya marudio itapigwa katika uwanja wa Uhuru ,jijini Dar es Salaam, Tanzania Oktoba 10.
Mshindi wa mechi hiyo atakabiliana na Ivory Coast katika raundi ya pili na ya mwisho huku timu saba zikifuzu kwa kombe la AFCON pamoja na wenyeji Misri.
Fainali za AFCON zitaandaliwa nchini Misri mwaka ujao huku pia mashindano hayo yakitumika kufuzu kwa michezo ya Olimpiki.