Timu ya taifa ya soka Harambee Stars itashuka katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo Jumamosi alasiri katika mechi ya kundi D dhidi ya Eritrea,kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka ujao.
Kenya ni ya 109 kwenye msimamo wa FIFA huku Eritrea ikikalia nafasi ya 184.
Itakuwa mara ya pili kwa Kenya kuchuana na Eritrea baada ya kuishinda Harambee Stars mabao 4-1, mwaka 2019.
Bafana Bafana ya Afrika Kusini itakabiliana na Guinea katika mechi nyingine ya kundi hilo mjini Durban.
Kenya wanatumia mechi hizo kujipiga msasa kwani tayari wamefuzu kama mojawapo ya waandalizi wa kipute cha mwaka ujao.