Wizara ya michezo imekiri kuwa imelipa marupurupu yote ya wachezaji wa timu za taifa za soka za Kenya na kuitaka Harambee Stars kuangazia mechi yao dhidi ya Eritrea, kufuzu kwa AFCON mwakani.
Kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya michezo tayari marupurupu yote ya awali yamelipwa kwa wachezaji na maafisa wa kiufundi wa timu za soka humu nchini.
Aidha,serikali imewataka wale ambao wangali wanadai marupurupu yao ya awali kuwasilisha malalamishi yao kupitia kwa njia zifaazo.
Vile vile,wizara imeitaka wachezaji wa Harambee Stars kujiandaa vyema kwa mechi yao ya kufuzu AFCON dhidi ya Eritrea mwishoni mwa juma hili.